Mwijaku: Mwanamke akikupenda na Kukuheshimu Bila Kuomba Pesa huyo ni ASSET, Mpe MTAJI.


Maana Mwanamke Bora anahitaji Mwanaume Bora na anayejielewa afu Mpambanaji haswaaa.... 

Mwanaume unatakiwa kuwa na ubongo wenye macho kujua wazo linakokwenda na masikio yenye mzani wa kupima kila kauli ,na moyo wenye utulivu kuweza kuwa na subira katika uwekezaji wa mapenzi.


Mtandao wa www.fortune.com umeonyesha thamani ya bei ya viungo vya mwanadamu.

Moyo una thamani ya $1.4 Million hizi ni sawa na Billion 3,246,600,000 za Kitanzania kwa hiyo unapompenda mtu kwa moyo wako wote jua umewekeza billion 3,241,062,369.86 returns ya uwekezaji wako inatakiwa furaha,amani, na vicheko.


Ukipempenda mtu hutakiwi kutoa hata Tsh 1,ukiona unampenda mtu harafu anaomba pesa kuanzia vocha ,kusuka,nguo vunja mkataba wa uwekezaji wa upendo wa billion 3 ,anza kujipenda mwenyewe.


Baadhi ya wanawake siku hizi ana degree lakini anaomba pesa za kufanyiwa birthday party,kwenda out na hana ajira wala wazo la biashara.Mwanamke wa aina hii liability hafai kwenye maisha wala ndoa ,sababu ana mbegu ya kuharibu kizazi.

Ukiona mwanamke haombi pesa kisha anakupenda na kukuheshimu jua huyo ni assets ,mpe mtaji kuwa muwekezaji mzuri kwake sababu mwanamke bora huwa na mume bora.Mwanamke wa namna hii ndio wajenzi wa familia wanaoendeleza vizazi.

Kuhonga ni udhaifu na kumhudumia mwenza wako ni jukumu lako ,kuna tofauti ya kuhonga na kuhudumia, mwanamke bora haombi pesa hata siku moja.



Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post