Wafahamu Kili Paul na Mdogo wake Neema Paul Watanzania Wanakiki India kwa Video zao TikTok | Nyota wa TikTok



Kutana na Kili Paul na Neema, Watanzania wenye asili ya Kimasai ambao wana-trend na kuviteka vyombo vya habari nchini India kwa kuimba nyimbo za kihindi.


Kili anajua kiingereza vizuri lakini hajui Kihindi licha ya kuimba vizuri kwa Kihindi. Mojawapo ya video yake iliyoteka India ni wanayoimba wimbo toka filamu ya Shershaah iliyotoka hivi karibuni na kufanya vizuri sokoni, filamu hiyo waigizaji wakuu ni Sidharth Malhotra na Kiara Advani ambaye kupitia Twitter ame-share pia video ya Kili na Neema wakiimba wimbo huo


Kampuni kubwa ya filamu Dharma Movies(Production) na Filmfare jarida namba moja la filamu nchini humo ambalo pia ni waandaji wa tuzo maarufu za Filmfare pia wameonesha kufurahishwa na Kili Paul na Neema


Kina Jubin Nautiyal waimbaji halisi wa wimbo huo pia wamefurahishwa na Kili na Neema


Tayari Kuna watu wenye asili ya Africa ambao walishapata nafasi ya kuimba nyimbo za kihindi zilizotumika katika filamu za kihindi kwahiyo usije kushangaa Kili Paul  na Neema wakaja kupata deal kwenye movie ya Shah Rukh Khan au Priyanka Chopra


Ukiachana na hilo, videos nyingi za Kili Paul hazifanyii filter hivyo kuvutia katika mazingira halisi yakiwemo ya jamii za kimasai mifugo ikionekana. Kili na Neema wameonekana kuwateka hadi wazungu wa mataifa mbalimbali. Wahindi pia wamejazana kwenye comments kumpa pongezi star huyo wa TikTok toka Tanzania. 

...........................

Kutoka BBC SWAHILI, Mastori kumhusu Kili Paul na Mdogo wake Neema Paul. 


.......Huku wakivalia vazi lao la kitamaduni la jamii ya Maasai na kuzungukwa na ng'ombe, nyota wapya wa Tanzania katika mtandao wa TikTok ambao ni ndugu Kili na Neema Paul, wanajiandaa kurekodi video yao hivi karibuni.


Simu ya smartphone inawekwa kwenye tripod mita chache mbali kutoka kwenye nyumba yao iliyopo katika Kijiji kidogo cha Mindu Tulieni, mashariki mwa jimbo la Pwani.


Mji uliopo jirani ni Lugoba, uko umbali wa saa moja kwa mwendo wa miguu. Kutokana na ukosefu wa umeme kijijini, Kili hulazimika kutembelea mjini ili kuchaji simu yake.


Wanajipanga vyema mbele ya kamera, Kili mwenye umri wa miaka 26, anasimama nyuma kidogo ya dada yake Neema, mwenye umri wa miaka 23.

Mara muziki unapoanza, ndugu hawa hugeuza midomo yao kuwa sawa kabisa na ile inayoonekana katika baadhi ya nyimbo na densi maarufu Bollywood.


Kwa kipindi cha miezi michache iliyopita, video za uimbaji wao wa nyimbo za Kihindi kwa namna iliyo sawa kabisa na waimbaji halisi zimekuwa zikisambaa sana kote nchini India na kuibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.


Video yao maarufu, iliyochezwa na Rataan Lambiyan kutoka filamu ya mwaka huu ya Bollywood Shershaah, ilitazamwa na watu zaidi ya milioni moja katika kipindi cha siku chache.

Wacheza filamu wakuu Kiara Advani na Sidharth Malhotra waliisambaza kwenye mtandao.


Muimbaji asilia wa wimbo huo, Jubin Nautiyal, aliwashitukiza ndugu hao kwa video hiyo wakati waliposhiriki katika mahojiano katika moja ya vituo vya redio vya India.


"Kila mtu anawafahamu nyinyi nchini India ,,"Nautiyal aliwaambia." Nyie watu ni maarufu!"


'Jambo la kushangaza'


Kutangaza kutoka Mindu Tulieni, ambako wengi wa wanakijiji hawana simu za smartphones, Kili na Neema hawakuwahi kufikiria kuwa video zao zitawafikia mamilioni ya watu nchini India na maeneo mengine ya dunia.


"Mwanzoni ilikuwa tu ni kujifurahisha, hatukudhani tutajulikana sana," anasema Kili. "Kwahiyo nilipoanza kuona kiasi cha watazamaji wa video na maoni kutoka kwa watu nchini India, nilishtuka. Haikuniingia akilini nilishangaa.


Kutengeneza video hizo kulitokana na mapenzi yao kwa filamu za Bollywood, ambazo Kili alizitazama kwa mara ya kwanza wakati alipokwenda kusoma katika mji mkuu, Dodoma.


Ingawa hakujua lugha ya Kihindi, yeye na dada yake wamejifunza kuimba kwa Kihindi.

Nyota wa TikTok Kili Paul: "Wazee mwanzo walijua labda nimerogwa"


Kijana wa kimasai kutoka Tanzania Kili Paul amejizoelea umaarufu katika mtandao wa TikTok baada ya kutumia mtindo wa kufuatisha mashairi ya nyimbo mbalimbali hususani zile za kihindi akiwa na mdogo wake Neema Paul


Kili na Neema Paul wamejizolea umaarufu mkubwa nchini India huku baadhi ya wasanii wakubwa wa Bollywood wakionesha kutambua kile anachokifanya.


Kili Paul anasema alipoanza kuchukua video hizi wazee wake hawakumuelewa na walifikia hatua hata ya kusema kuwa amepoteza akili au amerogwa kwani anachofanya ni kitu kigeni katika jamii yake ya kimasai.


BBC imezungumza nao, kutaka kujua walianzaje na manufaa gani wanapata kwa kuchapisha video zao mitandaoni?

...................

Zaidi Kuwahusu Kili Paul na Mdogo wake Neema Paul

Kili Paul ni Kijana mwenye asili ya Kimasai Alizaliwa Jumatatu tarehe 9 October, 1995 huko Umlazi, Kwazulu-Natal, na Kukulia Lugoba Mji uliopakana na Maeneo ya Pwani na Maeneo ya Mkoani Morogoro Tanzania ambapo ndio Makazi yake hadi sasa. Urefu wake ni Mita 1.85 na Uzito wa Kilo 85.


Kili Paul amezaliwa katika Famili ya Wakulima kwani Baba yake ni Mkulima na Mama yake ni Mtunza Familia, alimaliza Elimu yake katika Shule ya Sekondari ya Morogoro na akafanikiwa Kujiunga na Arusha Technical College kwa Masomo zaidi. 


Kili Paul ni Kijana Mwenye Ushawishi Mkubwa Kwenye Mitandao ya Kijamii, Dansa Mzuri, Mjasiliamali na Mzalishaji Maudhui ya Kimtandao yeye na Mdogo wake wa Kike Neema Paul ambaye mara Nyingi Umshirikisha Kwenye Video zake. 


Akiwa Mdogo alipendelea Sana Kucheza Mziki (Dancing).

Alipata Umaarufu baada ya Kuanza Kucheza, Kuimba na Kuigiza Nyimbo za Kihindi.


 Akiwa na Mdogo wake wa Kike Neema Paul, wametengeneza Video nyingi za Nyimbo MbaliMbali zilizokiki huko India hasa Nyimbo za Mastaa wa Kihindi kama Shah Rukh Khan, Salman Khan, Ayushmann Khurrana na Wengine.. 


Kili Paul anasema alianza Kupost video zake Mwaka 2019 kwa sababu ni kitu alichokipenda na kukifurahia lakini Umaarufu ulianza Kutokea Mwaka 2022 pale watu walioona Kipaji cha Tofauti. 


Anasema Wafuatiliaji wake wengi ni Watu wa India kwani wanapenda anachokifanya. 


Kili Paul na Mdogo wake wa Kike Neema Paul wamekuwa maarufu sana katika Mitandao ya Kijamii hasa TikTok, Instagram na YouTube, wanapata Heshima kubwa Kutoka India mpaka wameshafanyiwa Mahojiano na Media za India Online pia Kupewa heshima ya kutambua uwepo wao na Viongozi wa India nchini Tanzania. 


Vyanzo nilivyotumia kuandaa Maudhui haya ni BBC Swahili, NewsUnzip, Instagram Posts(Kili Paul). 



Focus Digito]


Follow Focus Digito] 


Home of Originals... No Copy and paste... Everything from Scratch. 


Acha ❤ ya Nguvu, tukupe Stori Mpya yenye akili. 


#FocusDigitoUpdates

From Instagram Posted by Focus Digito... Original Post. 


Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post