Ajira Mpya|Maelezo Ajira Wizara ya Afya Tanzania

 Wizara ya Afya imepata kibali cha kuajiri Wataalamu 1650 wa vitengo mbalimbali vya Afya ambao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi ambavyo vipo chini ya uendeshaji wa moja kwa moja wa Wizara ya Afya.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dr. Abel Makubi amesema huu ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.



Vitengo vitakavyonufaika na nafasi hizi ni pamoja na Madaktari Bingwa (25), Madaktari (215), Wafamasia(15), Maafisa Maabara(62), Wateknolojia (Dawa, Maabara, Mionzi, Macho-155), Maafisa Uuguzi (140).


Vitengo vingine ni 

Maafisa Uuguzi Wasaidizi (467), 

Wauguzi (140), 

Wakemia (2), 

Madaktari wa Afya Kinywa na Meno (15),

 Tabibu Meno (19), 

Watoa Tiba kwa Vitendo (15), 

Wazoeza Viungo kwa Vitendo(31), 

Maafisa Wazoeza Viungo (33), 

Maafisa Afya Mazingira(40), 

Wasaidizi wa Afya (134), 

Wahandisi Vifaa Tiba (17), 

Wateknolojia Vifaa Tiba (40)

 Watunza Kumbukumbu wa Afya (10)

 na Madereva (4). 



Source: MillardAyo 

Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post