History | Aliyopitia Mwanzilishi wa Kampuni ya Zoom | Zoom Meeting | Zoom Comferencing web

ERIC YUAN MWANZILISHI NA MMILIKI WA KAMPUNI YA ZOOM (Founder and C.E.O of Zoom Company).

Eric Yuan ni raia na mzaliwa wa China anayeishi marekani, ni mfanyabiashara , inginia na billionea.

Ni mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya Zoom Video communications. Utajili wake unakadiriwa kufikia Dola za kimarekeni Billion 17.

Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa C0VID-19, watu wengi duniani kote walianza kutumia zoom kama sehemu ya kufanyia mikutano, ndipo kampuni ilisuhudia ongezeko kubwa la watumiaji.

Yuan aliacha kazi yake aliyokuwa akifanya katika kampuni ya Cisco System ili kuanzisha kampuni yake. Kabla ya kwenda Marekani Visa yake ilikataliwa mara tisa 9 na alikuwa na uwezo mdogo sana wa kuongea kiingereza. Leo hii, yuan ni miongoni mwa watu matajiri duniani. Mwaka 2020, gazeti la “TIMES MAGAZINE” lilimtaja kama Mfanyabiashara wa mwaka yaan “Businessperson of the year”.

MAISHA YAKE NA UPAMBANAJI

Eric Yuan alizaliwa tarehe 20 February 1970 nchini China. Wazazi wake walifanya kazi kama Mainjinia wa giolojia. Alipokuwa darasa la nne (4th grade), Yuan alipendelea kukusanya mabaki ya ujenzi na takataka baadhi ili kuzitenegeneza katika vitu alivoweza kuuza na kupata pesa. Baada ya shule alifanikiwakujiunga na chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha  Shandong alipojipatia degree yake ya kwanza kwenye Hesabu. Katika kipindi cha mwaka wake wa kwanza wa masomo alifanikiwa kupata mpenzi au mchumba, ilimchukua masaa kumi 10 ya safari ya treni kwenda kumwona mpenzi wake kutokana na kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi mbali nay eye. Changamoto hii ilimchochea zaidi mpaka akafikia uamuzi wa kutengeneza mfumo utakaomwezesha kufanya mawasiliano ya kuonana kupitia mtandao yeye pamoja na mpenzi wake ili kutengeneza mazingira mazuri ya kuongea naye na kuonana naye. Kutokana na kuwa hili wazo lilikuwa ndani ya kichwa chake kwa muda mrefu ndipo alipoanzisha mfumo huo na kuuita jina kama Zoom. Baada ya chuo, Yuan alijiunga na chuo kikuu cha China alipofanikiwa kupata Masters yake kwenye Uinjinia wa geolojia (Geology Engineering).

Baada ya masters yake, Yuan aliingia mjini Beijing. Baadae akajiunga kwenye mafunzo ya muda mfupi huko Nchini Japani. Mwaka 1995, Bill Gates alitembelea Japani na alitoa jumbe nyingi nzuri ambazo zilimvutia na kumshawishi Yuan kuhamia Marekani (USA). Kabla ya kuingia marekani mwaka 1997, Visa ya Bwana Yuan ilikataliwa mara tisa 9 na katika kipindi hicho alikuwa na uwezo mdogo wa kuzungumza kiingereza kwa ufasaha hivo ilimpa shida sana kufanya mawasiliano katika mipaka ya nchi ngeni lakini bwana huyu hakukata Tamaa kabisa. Baadae bwana Yuan alijiunga na kampuni ya WebEx, mtandao ambao kazi zake kubwa ilikuwa ni kutengeneza na kuandaa mifumo inayolenga Mikutano kwa njia ya video (Video conferencing). Mwaka 2007, Yuan aliteuliwa kuwa makamu wa rais wa uinjinia. Ndipo mwaka 2011 alitoa wazo la la kutengeneza mfumo rafiki wa kutumia simu janja yaani smartphone kufanya mikutano kwa njia ya video na sio kompyuta pekee kama ilivokuwa awali. Lakini wazo lake lilikataliwa. Na sababu ya wazo lake kukataliwa ndiyo ilimsukuma kwa ukubwa kuacha kazi na kuanzisha kampuni yake binafsi ya Zoom Commuinications. Hii ni kutokana na kuwa alijiamini na alikuwana imani kubwa juu ya wazo lake.

IKAJA ZOOM,

Baada ya kuacha kazi kwenye kampuni ya Cisco System, Eric Yuan alianzisha kampuni yake ya mikutanao ya mtandaoni kwa njia ya video iliyoitwa Zoom Communications. Alifanikiwa kuachia software yake ya kwanza mwaka 2013 na ilipofika mwezi May, tayari ilikuwa na wafuasi au watumiaji million 1. Mwaka 2017, Zoom iligeuka nakuwa mfumo ulianza kutumiwa sana na watu mpaka kufikia billion 1. Kutokana na mlipuko wa C0VID-19 , Zoom ilishuhudia ongezeko kubwa la watumiaji duniani kote kutokana na kuwa kipindi hicho watu walizuiliwa kukutana ana kwa ana (LockDown). Katika kipindi cha miaka miwili tu, utajili wa bwana Yuan uliongezeka mpaka kufikia dola za kimarekani bilioni 17 na hii ikamfanya kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa nchini marekani.


 

Leo hii kampuni ya zoom inafikiriwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 35. Ndani ya miaka miwili mtandao huu ulikuwa kwa kasi na kuzipita Lyft na Pinterest. Mpaka leo hii nazungumza na kuandika hapa, Zoom ni mtandao unaotumiwa na makampuni pamoja na Taasisi karbia zote duniani kote kama njia ya kuwasiliana kupitia mikutano ya video ikiwa na uwezomkubwa wa kuwakutanisha watu popote pale walipo ukiachia mbali kigezocha umbali. Uwezo wa kutokata tama, uwezo wa kujituma na kufanya anachopenda ulimsaidia bwana Yuan kutenegeneza moja ya kampuni tajiri sana Duniani. Mara zote alijiamini yeye na ndoto zake zote. Mwaka 2020 gazeti la Times lilimwandika kama mfanyabiashara wa mwaka na wakaenda mabali sana kwa kumuingiza katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa mwaka 2020.

MATUMIZI YA ZOOM

Mpaka leo watu wanatumia mtandao wa zoom hasa katika Kuwasiliana kwa njia ya Video, Kufanya mikutano amabyo inaweza kuunganisha watu wengi isivyokawaida, Kutumiwa Mashuleni, Vyuoni, Maofisini , Mahospitalini na katika Taasisi nyingime au makundi mengine kufanya uwasilishwaji wa mambo yote yaliyo katika mfumo wa sauti, maandishi, picha na video, zaidi inatumiwa na wanafamilia kuwasiliana na kukutana wakiwa mubashara wakati mwingine watu wanaitisha vikaovya ukoo na mambo yanaenda sawa kabisa. Teknolojia inakua kwa kasi na sisi tukue nayo kwa kasi lakini kwa akili saana.

 

STORY YA ERIC YUAN.

Mwanzo kabisa, wazo la kuanzisha mtandao wa kufanya mikutano kwa njia ya video mtandaoni lilikataliwa. Akawaza mbali sana mpaka kuacha kazi yake kipindi hicho ili aweze kupata nafasi ya kupambania ndoto zake.


Hivyo hata sisi tunatakiwa kujiamini na kuziamini ndoto zetu bila kukata tama kabisa. Kufanya kazi kwa bidii ndio msingi na ufunguo wa mafanikio yoyote yale. Mwisho hii inatufundisha kujaribu kujifunza kupitia makosa yetu.

Nini maoni yako au kitu gani cha kuongezea zaidi katika historia ya bwana Eric Yuan?

Tuandikie katika comment nitapitia moja baada ya nyingine…nikipenda mawazo yako nitayaunganisha kwenye ukurasa huu.

Tukutane kwenye post mojawapo kati ya hizi hapa chini.

Tunakupenda .  

 

Suggested Video click here 



Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post