Cristian Ronaldo | Mama alikuwa Mpishi na Baba mtunza Bustani | Historia na Mapito yake


Jina kamili anaitwa Cristian Ronaldo Dos Santos Aveiro, alizaliwa February 5, 1985 huko nchini Ureno. Ni mtoto mdogo katika familia ya watoto wane – wakike wawili na wakiume wawili aliyekulia katika familia ya imani ya kikatoriki , kutokana na ugumu wa maisha alichangia chumba kimoja yeye, kaka yake na dada zake. Mama yake Maria Dolores dos santos Aveiro alikuwa Mpishi na Baba yake Bwana Jose Dinis Aveiro alikuwa Mtunza Bustani. Pamoja walifanya kazi kwa bidii ili kuhakisha familia inapata mahitaji yote muhimu.  Alipewa jina Ronaldo kutoka kwa jina la aliyewahi kuwa Rais wa Marekani Rais Ronald Reagan.

Alianza kucheza mpira akiwa na miaka 8 tu, mara nyingi alikimbia kukwepa  kufanya homework za shule.

Akiwa mtoto alipenda kucheza  mpira kuliko kawaida, ndipo alipata nafasi ya kuchezea timu ya Andorinha mwaka 1992 ambapo Baba yake alikuwa Mdau wa Timu hiyo.

Alikubaliana na mama yake kuacha masomo ili kujikita zaidi katika Mpira wa miguu.

Aliwahi kufukuzwa shule akiwa na miaka 14 kwa kosa la kumrushia kiti mwalimu huku akisema Yule mwalimu alimdharau.

Mwaka mmoja baadae alipimwa na kukutwa na Matatizo ya kiafya katika Mapigo ya Moyo ambapo alishauriwa kuacha kucheza Mpira hapo akiwa na umri wa miaka 15.

Alipoanza kujizoelea umaarufu aliomba kupewa t-shirt ya Namba 28 lakini alipewa Jezi namba 7 ambayo kwa miaka ya nyuma walivaa wachezaji nguri akina George Best, Eric Cantona na David Beckham. Baadae alipewa jina CR7 na alilazimishwa kuishi ndani ya heshima hiyo.

Ronaldo alikuwa mtu wa tofauti sana kwani alitumia nguvu na muda mwingi kufanya mazoezi ya mwili na Mpira, aliwashangaza wenzake aliporejea kambini kutoka likizo maana alipovua nguo katika chumba cha kubadirisha mavazi alionekana kuwa na kifua pamoja na misuli iliyotuna kwelikweli.

Ronaldo amezichezea timu kubwa kama Manchester United, Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno.

Ni mchezaji wa mpira wa miguu maarufu zaidi na anayelipwa pesa nyingi kuliko wote Duniani pia anaongoza  kwa kuwa na wafuasi wengi katika mtandao wa instagram.

Arnold Schwarzeneggar alimwita Ronaldo mwanariadha imara zaidi Duniani. Uwezo wake wa kuruka ni mara 5 ya wa Cheetah na spidi ya bao lake ni 13.1 kmph.

Mjini kwao amewekewa makumbusho (CR7 MUSEUM) ambako ndani yake kuna makombe, medali, picha na vitu vingine vinavyomtambulisha au kuhusiana na Ronaldo.

Ronaldo anachangia damu mara kwamara ,havuti sigara wala hana tattoo yoyote mwilini mwake.

Mali na mpira anatumia muda wake hasa katika kutoa misaada na kujihusisha na baadhi ya shughuli za kijamii.

Ufunguo wa maendeleo yake ulitoka kwa aliyekuwa meneja wake Alex Ferguson, ambaye baadae Ronaldo alisema “alikuwa baba yangu katika Mpira, mtu muhimu aliyenipa chachu ya kusonga mbele”.

“wengi tulicheza mpira kuwafurahisha wazazi wetu. Lakini Ronaldo ndoto yake haikuwa kuwafurahisha wazazi pekee bali kumfurahisha kila mtu aliyemtazama”.

 

Mpaka leo Ronaldo haitaji utambulisho kila mtu anamfahamu.

Nidhamu ni nguzo na siri kubwa ya mafanikio yake.

 




Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post