Story ya Binti aliye Nunua Gari kwa Boom la Chuo

 

Sikia hii, wakatumia Pesa ya Boom la Chuo wakanunua Gari na Kujenga Apartment... 


Ni katika kipindi kinachorushwa Kupitia Wasafi TV ambapo Binti Mmoja anayetumia jina la @nana_dollz alipofunguka kuwa alinunua Gari lake la Kwanza kwa kutumia pesa ya Boom la Chuo. Clip ya Video yake akizungumza maneno hayo ilisambaa kwa kasi sana mitandaoni na kuibua hisia za watu hasa Vijana waliopita Chuo kutahamaki kabisa Twitter, Facebook, Instagram hadi Tiktok, mtaani nako ilikuwa Story vijiweni.... 


Tukiacha na hiyo ikaja nyingine ya Jamaa Mmoja ambaye ni ni Mtangazaji wa kipindi cha SALAMA NA, anayetumia jina la "Daniel Kijo"


... wakati akizungumza alisikika akisema kuwa - "Boom la Chuo likitumiwa vizuri linaweza leta mafanikio makubwa sana tena sana kwa Wanafunzi... Tofauti na watu wanavyofikiri"



Aliendelea Kusema kuwa - yeye alipokuwa Chuo alikuwa anatumia hela ya boom kula bata na kununua TV lakini Kuna Rafiki yake wa karibu ambaye yeye alikuwa anajibana sana, baada ya muda alikwenda kuwaonesha Apartments (Mijumba) alizojenga kwa Hela ya Boom la Chuo. 


Sasa Ndugu yangu Seneta Mpambanaji kama wewe, Unahisi hii kitu inawezekana (Kwa Boom la Chuo Kufanya Maajabu ya Mafanikio) au Tunapigwa na vitu vizito kichwani... tunaambiwa yale tunayotakiwa kusikia na sio yale tunayotakiwa Kujua¿¿..... FUNGUKA nataka kujifunza kitu hapa. 

Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post