Mfahamu Khaby Lame Mchekshaji Maarufu TikTok na Instagram | Nilizaliwa Mwaka 2000


Anafahamika kwa jina la "Khaby", Jina Kamili anaitwa Khabane Lame. Alizaliwa Siku ya Alhamis tarehe 9 March 2000 Dakar Senegal. Ni kijana wa Kiislam, Msenegali kwa Kuzaliwa ila amekulia Mjini Chivasso, Turin huko Italia. 

....yote unayotaka kufahamu kumhusu Kijana Khaby Lame nimekuwekea hapa kwa Ufupi na Uhakika kabisa kuhusu Chimbuko lake, Vipaji ,Mchumba, Utajiri, Mitandao yake ya Kijamii na Mengine Yataongezeka kadiri muda unavyoenda...... 

Alijizolea umaarufu wake baada ya Kupoteza kazi yake ya Kuendesha Mashine Kiwandani kipindi cha Mlipuko wa Ugonjwa wa C0R0NA mwaka 2020.


Aliporudi Nyumbani kwa Baba yake alitumia Muda wake mwingi Kutengeneza na Kuposti vipande vya Video kwenye Mtandao wa TikTok. 


Kwa Vitendo tu bila kuongea Neno kwenye Video zake aliweza Kuvuta na Kuteka hisia za watu wengi kutoka Mataifa MbaliMbali Duniani. 


Alianzisha akaunti yake ya TikTok March 2020 kufikia April 2021 tayari alikuwa amepata Wafuasi Milioni 25.5 ndipo Umaarufu ulikua kwa Kasi Zaidi. 


Anasema "Watu unisimamisha mitaani na migahawani wakiniomba picha ya Pamoja (Selfie)"



Mbali na mambo ya Mitandao, Kijana Khaby ni Mchezaji Mzuri wa Mpira wa Kikapu na Timu yake pendwa ni LAKERS, anapenda Kusafiri na Rafiki zake, ni Mwanamitindo kama kipaji pia.

Kijana huyu wa 2000 ameshamchumbia Binti aitwaye Zaira Nucci, Mapenzi yana-run Dunia. 


Na sasa Kupitia Mitandao anapewa Madili ya maana yanayomwingizia Pesa ndefu takribani Dola za kimarekani Milioni 1.3 mpaka 2.7.



Kufikia Mwaka 2022 tayari alikuwa Mtu wa Pili mwenye wafuasi (Followers) wengi TikTok.


Data. 

TikTok = 136.7M Followers 

Instagram = 75.3M Followers 


From 

Focusdigito

Home of Originals. 

Instagram Posted by Focus Digito 


Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post