Historia Nzima ya Elon Musk Tajiri Wa Dunia aliyezaliwa Afrika Kusini


Jina kamili anaitwa Elon Reeve Musk FRS. Alizaliwa June 28, 1971 huko Mjiji Pretoria Afrika Kusini. Mama yake alikuwa Mwanamitindo na Mwanalishe mzaliwa wa Canada aliyeishi Afrika Kusini. Baba yake alikuwa Injinia wa Vyombo vya Moto, Rubani wa Ndege, Naodha wa Meli na pia aliwahi kuwa Mmiliki mwakilishi wa Kampuni ya Wazambia ya Kuchimba Madini karibu na Ziwa Tanganyika. Hivyo kumfanya Elon Musk kuwa na asili ya Afrika Kusini na Canada huku akiwa na Urahia wa Marekani. 

Alisoma Chuo kikuu cha Pretoria Afrika Kusini Miezi mitano tu Kabla ya kwenda Canada akiwa na Miaka 17. Baadae alijiunga na chuo kikuu cha Queen's na akahamishwa kwenda Chuo kikuu cha Pennsylvania ambapo alihitimu nakupata Shahada (Degree) yake kwenye Uchumi na Fizikia. Baadae alihamia Calfornia mwaka 1995 kusoma Chuo kikuu cha Stanford, ambapo badala ya Kusoma biashara aliacha Chuo ndani ya siku mbili tu na kuamua Kuanzisha Kampuni ya Zip2 akiwa na kaka yake. 


Elon Musk Ni Mjasiliamali, Mwekezaji na Mfanyabiashara Bilionea wa Kwanza Duniani akiwa na Utajiri wa Dola za kimarekani Bilioni 264.6 takwimu ya Forbes Mwaka 2022.


Elon Musk ni Mwanzilishi, Mkurugenzi, injinia, Msanifu Mwonekano na Mwekezaji wa Kampuni za SpaceX, Tesla, Neuralink na OpenAI. 


Elon Musk ni Baba wa Watoto 7 kama sio nane. Ambapo katika Mahusiano ametalakiana na Wake zake mara Tatu. 


Kwa Ufupi Mambo ya Kushangaza kuhusu Elon Musk

1. Aliacha Chuo ndani ya siku 2 baada ya kujiunga na chuo kwa ajili ya Kusoma PhD na Kuzindua Kampuni ya Zip2. 


2. Alimuoa mwanamke mmoja mara mbili yaani ameoa mara 3 lakini mara mbilu kwa mwanamke mmoja. 


3. Alitaja jina la mtoto na Kuhakikisha hakuna mtu mwingine anayeweza kulitamka. jina hilo ni (X AE A-12) 


4. Sio mwanzilishi wa Kampuni ya Tesla, alikuwa na Pesa nyingi baada ya kuuza kampuni ya paypal na kuwekeza Pesa hizo kwa Kampuni kama SpaceX na Tesla. 


5. Alizaliwa Afrika Kusini, Alianza kupata utajiri mwaka 1999 baada ya kuuza kampuni ya Zip2 kwa Dola za kimarekani Milioni 307.


6. Alivutiwa sana na hadithi za kisayansi na umeme kwani ndizo kazi kubwa baba yake alijishughulisha nazo zaidi. Akiwa na miaka 17 alikwenda Canada akitokea Afrika Kusini kusoma Fizikia na Uchumi. 


7. Mbali na Kuwa na Pesa Nyingi, lakini ameshawahi Kuachwa Mara tatu na wanawake. 


8. Aliweka Dau Kubwa kwenye Hisa za Mtandao wa Twitter kitu kilichomfanya awe Mtu aliwekeza hisa kubwa ziaidi na baadae akanunua hisa Zote za Kuwa Mmiliki Mpya wa Mtandao wa Twitter. 


"Anaweka imani Kubwa katika Ndoto zake lakini analeta Utani Mkubwa wakati wa Kuziwasilisha kumbe alishaanza Kuzifanya Kitambo" 


Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post