Kozi 10 za Chuo Zenye Soko, Fursa na Uhitaji Mkubwa Tanzania 2022/2023


Hizi ni Kozi zinazopewa Kipaumbele kikubwa likija Swala la Ajira na Fursa kutoka Serikalini, Mashirika, Taasisi binafsi na Makampuni bila Kusahau Nafasi au Upenyo wa Kujiajiri Mwenyewe baada ya Kuhitimu Chuo, Lakini pia Ukifuatilia kwa Kiundani zaidi ni kuwa Zinapewa Kipaumbele kikubwa kwa Wanafunzi husika Kupangiwa Mkopo na Bodi ya Mikopo Tanzania HESLB kwa sababu bado zinahitajika kwa Ukubwa Nchini. 

1. Kozi za Afya. 

Hizi zinaunganisha Kozi za utabibu kama Udaktari wa Madawa (Medical Doctor), Utabibu wa Meno (Dental Surgery), Utabibu wa Mifugo (Veterinary Medicine), Ufamasia (Pharmacy), Unesi (Nursing), Ukunga (midwifery), Sayansi ya Maabara (Laboratory Science), Teknolojia ya Mionzi Tiba (Radiotherapy Technology), Udaktari/utabibu wa Viungo (Physiotherapy), Utabibu wa Akili, na Teknolojia na Sayansi nyingine zinazofanana au kwendana na hizo. 

2. Kozi za Uandisi/Uinjinia. 

Hizi zinaunganisha Kozi Uandisi/uinjinia kama (Civil Engineering), (Mechanical Engineering), Uandisi wa Umeme (Electrical Engineering), Uandisi wa Uchimbaji, Uandaaji, na Uchakataji wa Madini, Mafuta na Vipuli, bila Kusahau Uandisi wa Kilimo na Vifaa Vifaa Vyake. 

3. Kozi za Ualimu. 

Hasa Ualimu wa Sayansi kwani walimu wa Masomo ya Sanaa wengi Mtaani na idadi yao ni kubwa kila Mwaka wakuhitimu. Lakini pia Kipindi hiki walimu wa Sayansi wameongezeka pia unakuta wanahitajika sana Lakini kwa nafasi zinatolewa chache sana. 

4. Kozi za Sheria, Kanuni na Sera za Nchi. 

Hapa nawazungumzia wanasheria (Law and Enforcement) , Mawakili (Advocates) na wengine wanaoendana na Kozi hizo. 

5. Kozi za Kilimo, Misitu, Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji. 

Agriculture, Forestry, Wildlife Management and Conservation, Reserve. 

6. Kozi za Sayansi na Utaalamu wa Kompyuta, Mifumo na Mitandao. 

Computer Science, Application, Websites, Software and System development, Databases, 

7. Kozi za Utawala, Biashara, Masoko na Rasilimali.

Political science, Human Resources management, Business administration, Marketing, Public relations and administration. 

8. Kozi za Uzalishaji Maudhui katika Mfumo wa Machapisho, Maandishi, Sauti na Picha + video. 

9. Kozi za Ufundi, Mawasiliano, Usafirishaji Utamaduni na Utalii. 

Technicals, Transport and Communication, Travel, Tourism, Cultural Heritage 

10. Kozi za Uhasibu na Fedha. 

Accountancy, Finances, Procurement and Supply.

Wakati Mwingine ni Vema Kuangalia Kitu gani kinapewa Kipaumbele kuliko Kufanya Unachokipenda na akipewi Kipaumbele sawa na Msanii kuwa na Nyimbo Nyingi alafu hazitrend Mtaani wala Mitandaoni sasa Msanii huyu atatoboa Lini. 

Fahamu kuwa Kila Mwaka Serikali uweka Malengo ya Kuzalisha au Kuandaa Wasomi, Wataalamu na Wabobezi kutoka Sekta Tofauti na hapo ndipo Vipaumbele uzaliwa na Hivyo Vipaumbele vinakuja Kwenye Kozi na Kozi zinategemea Taasusi au Combination ulizosoma ukiwa Advanced Level PCB, PCM, PGM, CBG, CBN, CBA, EGM, HGM, HGE, HKL, HGK, na Kombi Nyingine Nyingi. Kwani Kuna Uwezekano watu wawili wakasoma Kitu kilekile lakini wapo kwenye Kozi Tofauti ndani ya Faculty /idara Moja.



Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post