Kijana Elliot Tanner Kupata Degree Ya Kwanza akiwa na Miaka 13 Chuo Kikuu Cha Minnesota Huko Marekani


 Jina Kamili anaitwa Elliott Tanner alizaliwa Mwaka 2005 huko Marekani. Katika Ukuaji wake alipendendelea Kufanya majaribio ya Fizikia kwa Vitendo na Nadharia, Hesabu na Kutengeneza mifumo ya Kompyuta. 


May 2020 Kijana Elliott alihitimu Chuo cha Kati akiwa Umri wa miaka 11 aliposomea Sayansi ya Hesabu na Kupata Daraja la Heshima akiwa na GPA ya 4.0. Baadae alipata nafasi ya Kusajiliwa katika Chuo Kikuu cha Minnesota huko Marekani katika Idara ya Sayansi na Uinjinia ambapo atahitimu akiwa na Shahada (Degree) ya Sayansi katika Fizikia na Hesabu Mwezi May, 2022.


Ripoti Kutoka idara ya Taaluma inasema katika Matokeo Yake ana wastani wa GPA ya 3.78. 


Zaidi ni kwamba tayari amekubaliwa Kusoma PhD ya Fizikia ya Chuo Kikuu cha Minnesota na ana mpango wa kuwa mwanafizikia wa nadharia ya juu na kuwa profesa shuleni


alisema "Nina shauku ya ajabu ya fizikia,imekuwa moja ya mambo ninayopenda kufanya."


Tanner alianza kusoma na kufanya mazoezi ya somo la hesabu akiwa na umri wa miaka 3, kulingana na maelezo ya mama yake Michelle Tanner, alimaliza masomo ya secondary na shule ya upili katika mda wa miaka 2 tu na kuanza chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 9 baada ya kusomea nyumbani kwao.


Mbali ba kusoma, Kijana Elliott anapendela Kushiriki michezo na Familia, kucheza michezo ya Mitandaoni na Rafiki zake kama Minecraft, Kusoma Vitabu, Kusafiri na Kusikiliza Muziki hasa Nyimbo za - the Beattles na Billy Joel. 


Hata kwa mafanikio yake ya ajabu, kijana huyu hatokuwa Mhitimu mdogo zaidi wa Chuo Kikuu kikuu, Cheo hicho kinashikiliwa na Michael Kearney, ambaye alipata stadhahada yake ya kwanza katika somo la anthropolojia kutoka Chuo Kikuu cha Alabama Kusini nchini Marekani mwaka 1994, alikuwa na umri wa miaka 10 tu.



Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post