Lifahamu Jiji la Dar es Salaam na Historia Yake|Jiji na Mji Mkuu wa Kiuchumi Tanzania


Dar es salaam ni Mji wa kiuchumi/kibiashara nchini Tanzania. Ni Jiji lenye Bandari makini katika fukwe za bahari ya Hindi. Mji huu ulikua kutokea kwenye Kijiji cha Wavuvi miaka hiyo. 


Dar es salaam ni neno la Kiarabu lenye maana ya 'Abode of Peace' Sehemu ya Amani. 

Mji huu ulianzishwa na kuzinduliwa mwaka 1862 na aliyekuwa Sultan wa Zanzibar (Sultan Majid bin Said) kutoka kuwa Kijiji cha Mzizima na kuwa Dar tunayoijua.


Umaarufu wake ulianza kukua Zaidi pale Wajerumani walipojenga Reli iliyoingia Mpaka Kigoma. 


Jina lingine (Nickname) inaitwa 'BONGO', jina la Kiswahili litokanalo na Neno 'Ubongo' kutokana na kuwa Watu waliotokea Dar es salaam walionekana kuwa na Akili Kubwa ya Maisha na Utaftaji... harakati za Mtu Mweusi, Harakati za Mbongo. Ukitaja Bongo Utajikuta unaongezea na Fleva ili kuleta Neno BongoFleva ambayo ni aina ya Muziki flani hivi Wenye Mjumuiko wa Hip-hop, RnB, Reggae na Muziki wa Asili ya Kitanzania kama Dansi na Taarabu. 


Dar es salaam kilikuwa kijiji cha Wavuvi kilichovutia wakazi wengi kutoka tamaduni MbaliMbali Tanzania mpaka kufanya Dar kuwa na mchanganyiko mkubwa wa Tamaduni na Makabila ya Tanzania na Nje wote wakiwa katika Mfanano wa style za Maisha. 


Ukubwa wake ni 1,590Km² na hali ya hewa mara nyingi ni 27degree C. Inakadiriwa kuwa na Wakazi wanaofika Milioni 5, ikiwa na Wilaya zake kama Ilala, Kigamboni, Kinondoni, Ubungo, na Temeke. Code yake ni O22. 


Gharama ya Kuishi Bongo Dar es salaam sio Kubwa sana ni Rafiki kwa Binadamu yeyote. 

-Kwa Familia ya watu 4 kwa mwezi inakadiriwa kufikia kiwango cha Juu cha Matumizi ya 3,708,173Tsh.

-Kwa Familia ya Mtu mmoja Kw Mwezi kiwango cha Juu cha Matumizi kinaanzia 1,080,934Tsh.

(Chanzo - Numeo.com).


Kukosa Kazi ya Kufanya ukiwa Jijini Dar es salaam ni wewe umetaka. Lakini Kupata kazi nzuri yenye maslahi inahitaji connection na uwe mtu wa Kujichanganya sana na Watu pia Mwepesi wa Kuchangamkia Fursa. 


Kuwa na Msongo wa Mawazo jijini Dar ni wewe umetaka, kwani kuna Maeneo Mengi ya Kujivinjali na Kutuliza Ubongo, Fukwe Z Kutosha, Starehe kibao. 


nikupe nafasi ya Kuongezea Nyingine wewe unayeifahamu Dar es salaam... kazi kwako. 

Tembelea www.focusdigito.com upate zaidi. 


Tufuatilie katika Mitandao ya Kijamii Instagram, facebook Twitter... 


YouTube channel /Focus Digito 


Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post