Stori Zote - Kifo cha Swalha Aliyeuawa kwa Kupigwa Risasi na Mume wake akajiua pia

 

Alijulikana kwa Jina la Swalha-Mwanamke maarufu jijini Mwanza, aliyekuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make up artist) aliuawa kwa kupigwa risasi na mumewe usiku wa kumkia Jumapili ya May 29. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu.

 (👨‍🏫Jitahidi kusoma Mpaka Mwisho, Maana kama wewe ni Mvivu wa Kusoma hautaweza Kuelewa Chochote, kila kitu kimeandikwa). JITAHIDI KUSOMA..... 

Watu wa karibu wanasema kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. 

Lakini pia Mume wa Swalha alikuwa na Kasumba ya Kuleta Ugomvi na kumpa Kipigo Mke wake mara kwa mara. 

Ugomvi ulipoanzia:-Swalha alienda kuangalia mpira na akachelewa kurejea nyumbani. Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani hivyo kukazuka ugomvi baina yao hali iliyopelekea mume wa Swalha kumfyatulia risasi.

🤔 Kwenye Mahusiano na Ndoa za watu kuna Siri Nyingi sana na mara nyingi huwa azitajwi kukishatokea Migogoro bali zinaunganishwa kwenye sentensi moja kama Wivu wa Mapenzi, na Lawama nyingi kuwaangukia Wanaume kutokana na Maamuzi yao ya ajabu. 


📝 Jamii hasa Vijana wanashindwa Kujifunza mambo mengi kuhusu Mapenzi kutokana na kuwa hakuna anayetaka kutaja Exactly viini vya Ugomvi, badala yake yanatrendi Matokeo ya Ugomvi kama vifo, majeraha, maumivu, vilio na kadharika.... Watu wanakufa kutokana na Ukimya wa Muda Mrefu, UKWELI UNAPONYA, UKWELI UNAWEKA WATU HURU. kwani hakuna anayetaka kuonekana Mbaya baada ya Upendo kufa. 


📝 Kuna NGOs Nyingi sana zinazosimama upande wa Watoto wa Kike, watoto wakiume wanasahaurika. Kila siku Swala anafundishwa namna ya kumkwepa Simba lakini Simba hana wakumfundisha kumwelewa Swala. Matatizo hayawezi kuisha pasipokuwa na Win-to-Win Situation.

Wanao Ujua Ukweli Wamefariki, Zilizobaki ni Stori Tu. Wawili hao (Bwana Said na Bi Swallher) ndio wangekuwa Chanzo kikubwa cha Habari kwani Ukweli wote wanaujua wao,  wengine wanaongea kulingana na walichosikia, walichokiona na walichokisoma kwenye Mitandao ya Kijamii na Ushahidi wa ndugu na Majirani.

Matukio Mengine yanatokea kwenye Jamii ili Tujifunze. Cha Ajabu ni kuona ajari zinatokea kila Siku lakini watu hawaachi kusafiri. Tanzania hii kuna sehemu mtu anapitia kama haya yanayosemwa lakini yupo kimya huko. 

Kwenye Mahusiano na Ndoa - "Mwanamke anataka Upendo wa Kweli, Mwanaume akiheshimiwa Vizuri na Mwanamke anatafsiri Heshima kama Upendo".
Mwanaume ameandikiwa - aishi na Mke wake kwa Akili.

📝 "Binafsi mimi nina mtazamo tofauti na hii ishu ya hawa bw said na bi swalher.
Nimesikiliza interview za mama yake zote, wadogo zake wote inaonyesha swalher alikua ameolewa kwa ajili ya pesa sio mapenzi hakumpenda wala kumuheshimu mumewe na alikua anacheat.

Mumewe kasafiri kwenda ukerewe na yeye nyuma Kasafiri kaenda kupamba shinyanga ,kamaliza kazi hakurudi nyumbani Kalala huko kasema kapata kazi nyingine ya kupamba,anapigiwa simu hapokei then anarudi nyumbani hakukaa kumsubiri mumewe kaenda mpirani, mume karudi nyumbani mke hakumkuta anampigia simu hapokei ...japo mama yake kasema simu iliisha chaji lkn mdogo wake kasema alikua hapokei kwa sababu mumewe alikua anamtukana, anarudi nyumbani anamkuta mumewe na km unavyojua wanawake hawa wanaojiona wazuri lazima atakua kamjibu mumewe ndivyo sivyo jeuri na dharau nyingi ....mwanaume kaamua alivyoamua.

Japo haipendezi kujichukulia sheria mkononi lkn kwangu mimi swala lk la kujiua kwangu ni la kishujaa sana maana km angekua hai na kukamatwa basi pesa zote na mali zote zingeteketea na familia yake hasa Watoto wangeteseka. Wanaume wakipata hela huwaga wanaangaika sana na ulimwengu" - Aliandika Mtanzania mmoja kwenye Ukurasa wake wa Instagram. 

TAARIFA IKATOKA RASMI. 
Mwanaume mmoja Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) naye amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi

Makori amethibitisha kujiua kwa mtuhumiwa huyo

ambaye mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa

Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza.

"Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Timejiridhisha kuwa ndiye mtuhumiwa baada ya kutambuliwa na ndugu zake," amesema Kaimu Kamanda huyo.

Amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.


Mtangazaji wa Kike DIVA aliandika:- Very sad, Huyu Dada @iam_swallher aliuliwa Usiku wa Kuamkia Jumapili Na Mume Wake anaeitwa (Said Oswayo)* kwa Kupigwa Risasi 7 Kichwani na kufariki hapohapo, alikuwa Maarufu Kwa Mkoa wa Mwanza kwa urembo wake lakini Pia alikuwa Make Up artist Maarufu Jijini humo, Kisa Cha Kufikia Mauaji hayo inadaiwa ni wivu wa Kimapenzi,

Mwanaume baada Ya Kufanya mauaji hayo alikimbia (na baadae naye akajiua kwa Kujipiga Risasi) -added*

Wasifu wake ni inasemekana ni mfanya biashara maarufu na anaejiweza kifedha na mara kadhaa alikuwa akimpiga dada huyu na kumtishia kuwa kuna siku angemiminia kichwani risasi, wazazi walihusika kuwasuluhisha na mara kwa mara alivumilia na kurudi kwa Mume wake, kuna siku alipigwa na kitako cha bunduki na kuzimia Masaa matatu mazima. 

Mwenyezi Mungu amuweke Mahali Pema Amina!. 

Wanawake wenzangu Pls say NO to Violence. ondoka kabisa.

Anaekupenda ata awe amekuoa kama anakupenda toka Moyoni hawezi kukurushia ata kibao, hawezi kukunyanyasa na hawezi kukupiga!.

Ukatili wa majumbani umekuwa mkubwa sana na vyombo husika huchukulia kawaida suala hili, wazazi nyie pia ni chanzo kikubwa kwa kusema ndoa inahitaji uvumilivu au mtu akipingwa ndio Mapenzi rudi kwa mumeo mbona baba yako tunavumiliana Jaman kuna talaka iwapo mtashindwana iliwekwa sababu ya kuepuka vitu kama hizi, Huyo Mwanaume amezima ndoto za dada wa watu, Kama Wewe ni Mwanamke na una face hii hali Pls file a Report usije fikwa na umauti hakuna Mapenzi Ya Kupigana, Nawaombea wote mnaopitia Manyanyaso kusema Hapana kwa ukatili huu,
Hii Haikubaliki kabisa.

Naandika nikiwa najisikia vibaya sana kwa kuondokewa na moja kati Ya Followers wangu. Mwanamke Mwenzangu na Mtanzania Mwenzangu, Pole ndugu na Jamaa kwa msiba huu.

Pumzika Kwa amani Mpendwa!. RIP beautiful.
-Alimalizia kuandika @divatheebawse Mtangazaji #wasafifm

Wewe kama Seneta Mpambanaji unasemaje, Nini maoni yako¿¿.... ❤💔

Tukutane YouTube, facebook, Instagram, twitter, TikTok na Google kwa Jina la Focus Digito. Dunia yetu sote. 

Follow @focus_digito 


Mwanadada Maarufu Nchini Tanzania anayefahamika kwa Jina la CAPPUCCINO TUNDA (BossBabe), baada ya kuguswa na Tukio la kuuwawa kwa Swalha huko Mwanza, Tunda amefunguka na kuandika kilichowahi kumkuta na kinafanana na kilichomkuta Bi Swalha.

Anaadika Tunda :- 
R.I.P beautiful!..nimeskiliza hii story hadi mwili umenisisimka aisee!..

Aya mambo yapo kweli imenikumbusha nyuma huko na mimi nilishawahi kuwa kwenye mahusiano ambayo nikikosea kitu hata kama sio kikubwa cha kuongea tu au alikua akihisi tu kitu ni napigwa hadi nashikiwa bastola sio mara moja wala mara mbili lakini mimi ni muoga sana ilinipelekea kuacha kila kitu na mapenzi yote niliyokuwa nayo lakini nikaona hapana inabidi nitoke huku iki ni kifoooo!..

Jamani uhai ni zawadi ambayo huwezi kupewa mara mbili ikiisha imeisha haiwezi kurudiwa!..

Tuweni sana makini na awa tunawaita maboyfriend au wanaume zetu ukiona kama kuna vitu haviko sawa aisee ni bora uachane huko!..
Pia hata serikali hawa watu wanakabidhiwa silaha inabidi wachunguzwe sana jamani watu Wanapoteza familia zao ni huzuni sana aisee sio kikawaida kama tunavosoma tu juu huku mitandaoni!.. 

Mungu atupe mwisho mwema kila mmoja wetu!..
Mapenzi ni furaha na burudani isiwe sababu ya maumivu kwa familia zetu. Anamalizia @cappuccino_tunda

Lazima kuna mabinti au wanawake ambao wanatishiwa au waliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola kwenye Mahusiano, Uchumba au Ndoa na Waume zao, Boyfriend zao au Wapenzi wao ila walikaa kimya na kupotezea na wengine wapo kimya wanaugulia Maumivu huko mpaka Muda huu na hawana cha kusema. 

Tuchague Kujifunza kupitia Makosa ya wengine ila tuombe sana yasitukute sisi. 

Wakati Mwingine Hofu ya Mungu inatosha kumaliza Matukio ya Ajabu kama Mauaji, ubakaji, ulawiti na mengine. 

Follow @focus_digito 

Tukutane YouTube, facebook, Instagram, twitter, TikTok na Google kote kwa Jina la Focus Digito tuelimike zaidi. 

#FocusDigitoUpdates

Endelea kusoma zaidi ili uweze Kuelewa zaidi... 
FUNGA KAZI HII HAPA.......
Sasa kwanza tumjue vizuri mwanaume.
Jina lake kamili anitwa Said Oswayo
Nimeingia kwenye file zake za nyuma na kubaini kwamba huyu jamaa amewahi kufanya kazi Geita Mgodini kwa miaka kadha kisha file lake la 2019 inaonesha alikuwa na kazi visiwani ya kuuza samaki.

Kwenye file la Afya sijabahatika kuona kama jamaa alikuwa na tatizo la Afya ana umriki halali wa Bunduki no : 

" Sasa mnamo " 30,December 2021 Mwanaume alikwenda kufunga pingu za maisha ili iwe halali kabisa kuwa mme na mke sababu ilikuwa uswahili umezidi kwa mwanamke mara kile mara hiki " hivyo jamaa akaenda katoa mahali wakafunga ndoa kilaini kabisa.

Mwanamke ambaye ni marehemu kwanza kwa miezi 3 wamo kwenye ndoa alikuwa hataki na anagoma kupika chakula waliokuwa wanapika ni vijana wa kiume pale nyumbani" 

Utana kabisa "Siku moja marehemu kafunga safari kwenda Shinyaga akiwa huko bila hata ruhusa ya mwanaume wala kumwambia chochote akalala huko zaidi ya siku 3 bila taalifa mwanaume akipiga simu mwanamke anamkatia simu na kuweka simu hadi miscall 56 "

Juzi Diamond akiwa Mwanza, 
Mwanamke kaamua kabisa kujipodoa vizuri wakati huo mwanaume yupo kazini kisiwani kabisa anapata taalifa kuwa mwanamke anatoka kwenda kwenye tamasha la Mziki wa Diamond na hapo Ndoa ina miezi 5 bado, Mwanaume akamwambia hakuna kwenda sahivi unafaha ubadilike usha kuwa mke wa mtu , mwanamke alichokuja kujibu baada ya hapo ilikuwa kwani kumwoa kitu gani, kwani siwezi kwenda kufurahia na narafiki zangu kipindi anaongea hayo taalifa za kuaminika alikuwa ameongozana na mpenzi wake wa zamani kavali nusu uchi na make up zake usoni ,

Mwanaume akamwambia sasa wewe nenda atakaye kuja kukufungulia geti ni bastora za kichwa ,
Mwanamke kiutaniutani akasema usinitishe na kuniua kila siku unanitishia mimi sikuogopi Bwana niache kwenda naenda na hunipigi kabisa, Aya aya simu zikakatwa.

Huyu ambaye mnamwita muuaji hasira zikapanda washikaji zake pale akawaaga akawaambia aki ya mama huyu mwanamke kazidi naenda kumfanya kitu mbaya wewe na ilikuwa mchana acha jamaa achanize Mbuga hadi Busweru Mwanza mpaka camera zangu zinanasa ilikuwa amefika majira ya saa 11 jioni alikuwa amevalia suluali nyeusi hivi.

Nimedata hapa,....
Mwanamke kafungua geti hivi 
Anakutana nayo .paaaaa ya kwanza
Paaaa 2
Paaaa3
Paaaaaa4,5,6 na ya 7 mtu kimnya kama maji ya mtungini, kwenye pochi alikuwa na 76,000 

Nasikitika sana kuona 
Kijana huyu akajenga nyumba nzuri 
Kampa mwanamke uhuru wa gari zaidi ya 3
Kampa ruhusa ya kazi wengine hawana.

Ila mwanamke hadi anaenda kulala kwa mama yake siku 4 mwanaume gari inakwama njiani anamwomba mwanamke awahi home kupika chakula anakuja kula mwanamke anagoma hadi mama yake anamwambia wewe nenda kwa mme wako kanipigia simu hii mara ya 7 mwanamke hana haraka wala shida naombeni jamii hasa wanawake mnijibu hivi mwanamke na mwanaume nani alijisahau hapa  Wajibu na majukumu yake ......???



......ALIANDIKA MTANZANIA MMOJA..............
 



Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post