TAMISEMI|Taarifa Ajira Kada ya Afya na Elimu 2022 | Miaka inayopewa Kipaumbele |Maelekezo

Ofisi ya Rais - TAMISEMI ilitoa Tangazo la Ajira 9,800 kwa Kada ya Ualimu na 7,612 kwa Kada ya Afya, Tangazo lilitolewa mnamo tarehe 20.04.2022.

Kufuatia Tangazo hilo, waombaji wa ajira hizi wamewasilisha changamoto mbamblimbali ambazo ufafanuzi wake ni kama ifuatavyo:


1. Mfumo wa Ajira kutofunguka - Kwa sasa mfumo wa ajira unafanya kazi vizuri kwa kasi ya kutosha na mpaka tarehe 25.04.2022 saa nne usiku waombaji wa Kada ya Ualimu walikua 69,813 na Kada ya Afya ni 13,683. Jumla ya Waombaji wote ni 83,514. Waombaji wote hawa wameomba kupitia mfumo ajira.tamisemi.go.tz kwa muda wa siku tano tu. Hivyo ni takribani waombaji 16,703 huwasilisha maombi kwa siku.


Waombaji ambao bado wanakutana na changamoto mbalimbali kama ni za kimfumo waangalie zaidi mtandao wanaotumia, eneo walilopo na taarifa wanazoingiza kwenye mfumo. Aidha, wahakikishe kuwa taarifa zao ni sahihi na wanatumia mtandao wenye kasi wakati wa uingizaji wa taarifa katika mfumo.


2. Kigezo cha Mwaka kwa ajira za Kada ya Ualimu kuanzia mwaka 2015-2021- Hii ni kwamba wahitimu wa miaka ya nyuma wengi waliajiriwa moja kwa moja Serikalini na wale waliokuwa wamebakia na wana sifa waliajiriwa kwenye Ajira zilizotangazwa mwaka 2018 - 2021 hivyo kwa sasa tunaendelea na wahitimu ambao walianza na mfumo wa kutoajiriwa moja kwa moja Serikalini ambao ulioanza kufanya kazi mwaka 2015.


3. Kugonga Muhuri vyeti vya Kitaaluma - Hiki sio kigezo muhimu katika uombaji wa ajira hizi unaweza kuomba bila kugonga muhuri kwa Mwanasheria na maombi yako yakapokelewa na kufanyiwa kazi.


4. Lugha inayotumika kuandika barua ya maombi - Waombaji wanaweza kutumia lugha yeyote (Kiswahili au kingereza) kutuma maombi yao.


5. Wasifu - Hakuna sehemu ya kuweka wasifu kwenye mfumo wa ajira hivyo waombaji wote wafuate maelekezo yaliyopo kwenye mfumo.


6. Waombaji kujisajili upya - Waombaji wote wanatakiwa kujisajili na kufungua akaunti mpya hata kama alishawahi kuwa na akaunti aliyotumia kuomba ajira zilizopita ndio aendelee na maombi ya ajira za mwaka 2022.


7. kutoonekana kwa baadhi ya Mikoa na Halmashauri wakati wa kuchagua kituo cha kazi - kwa sasa Mikoa na Halmashauri zote zenye uhitaji wa watumishi wa Kada ya Ualimu na Afya zinaonekana kwenye mfumo: Kwa wale waliokutana na changamoto hii hapo awali wanaweza kujaza tena kipengele hiki.


8. Baadhi ya kozi kutokuwepo kwenye mfumo - Kwa sasa kozi zote za vyuo vilivyosajiliwa TCU na NACTE zimewekwa kwenye mfumo kama utaendelea kukutana na changamoto hii wasiliana na kituo cha huduma kwa mteja kwa msaada zaidi.


9. Kutoonekana kwa somo moja la kufundishia - Kwa mujibu wa kibali cha Ajira masomo yote yaliyopata kibali yameingizwa kwenye mfumo kama utakua huoni somo la pili la kufundishia itakua somo hilo halipo kwenye kibali cha Ajira.


10. Kufuta taarifa uliyoiweka kimakosa/uliyokosea - Kama umeweka taarifa ambayo unadhani unataka kuifuta mfumo umewezeshwa kuweza kuondoa taarifa hiyo na kuweka nyinginge mpya.


11. Unapopata ujumbe wa 'something went wrong contact the system admin' wakati

wa kutumia mfumo - Ujumbe huu unatokana na shida ya mtandao. Muombaji anashauriwa abadili mtandao/network na kujaribu tena. Mara nyingi huwa si tatizo la kuduma iwapo mawasiliano yatakuwa vizuri.



Chanzo : Tamisemi 

Admin-01

"You Can't be successful by just taking Easy Options"

Post a Comment

Leave a Comment, Tell us and the Audiences in Focusdigito.com anything in your Mind Today.

Previous Post Next Post